Home » » TFDA yateketeza dawa zenye thamani ya MAMILIONI

TFDA yateketeza dawa zenye thamani ya MAMILIONI

 Mamlaka ya Dawa na Chakula Tanzania (TFDA), Kanda ya Kaskazini juzi iliteketeza dawa, vyakula na vipodozi vya aina mbalimbali vyenye thamani ya zaidi Sh6.9 visivyofaa kwa matumizi ya binadamu vilivyokamatwa kwenye operesheni maalum iliyoendeshwa jijini Arusha.
Meneja wa TFDA, Kanda ya Kaskazini, Damas Matiko alisema bidhaa hizo zilikamatwa kutoka katika maduka mbalimbali jijini Arusha wakati wa oparesheni iliyoendeshwa na mamlaka hiyo kati ya Juni 10 na Juni 27, mwaka huu.
“Pamoja na kukosa usajili kutoka TFDA, baadhi ya bidhaa tulizokamata zilikuwa zimeisha muda wa matumizi, maelezo kuandikwa kwa lugha isiyoeleweka kwa walaji, kupigwa marufuku nchini na kuharibika vifungashio,” alisema Matiko.
Meneja huyo alisema shehena iliyokamatwa na TFDA ilikuwa zaidi ya nusu tani huku vipodozi na dawa zikiwa na idadi kubwa ikifuatiwa na vyakula vya aina mbalimbali zikiwamo juisi, mivinyo, pombe kali, unga wa sembe na ngano pamoja na mafuta ya kupikia.
Katika oparesheni hiyo, TFDA ilishirikiana na taasisi na mamlaka nyingine wakiwamo polisi, wataalamu wa Idara ya Afya kutoka Jiji la Arusha na mazingira
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan Tanzania Mpya untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Hisia za Mwananchi

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2013. Tanzania Mpya - All Rights Reserved
Template Modify by Hisia za Mwananchi
Proudly powered by Hisia