Showing posts with label Teknolojia. Show all posts
Showing posts with label Teknolojia. Show all posts

UTAFITI: Haya ndiyo madhara ya kutoa mimba kwa wanawake, Wizara afya yasema, inasababisha kansa ya shingo ya uzazi

Utafiti mpya uliofanywa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii umeonyesha kuwa kutoboka kwa kibofu cha mkojo, kushamiri kwa kansa ya shingo ya uzazi, utasa na matatizo ya kisaikolojia kwa wanawake kunatokana na kasi kubwa ya utoaji mimba nchini.



Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Mtumwa Mwako, akizungumza mjini hapa jana, alisema ripoti ya utafiti huo inaonyesha kwamba, utoaji mimba ndiyo  chanzo kikuu cha matatizo mengi kwa wanawake.
Alisema licha ya mara nyingi utoaji mimba kufanywa na watu wenye utaalamu katika sekta ya afya wakiwamo wauguzi na waganga wanaokiuka maadili ya kazi zao, vitendo hivyo vinafanyika kwa usiri mkubwa.

“Kwa mujibu wa tafiti hiyo, wakati wa utoaji mimba kuna uwezekano mfuko wa uzazi kutobolewa, vipande vya mwili wa mtoto anayetolewa  kubaki tumboni kutokana na haraka na kukosa ujuzi, hali ambayo yaweza sababisha  mauti kutokana na kutokwa kwa damu nyingi wakati wakitendo hicho” alisema Dk. Mwako.

Alisema pia mtoaji mimba anaweza kushindwa kubeba mimba  nyingine kutokana na mimba  hizo kutunga nje ya kizazi na  kuharibika muda mfupi baada ya kupata ujauzito.

Aliwataka vujana wa kike kuacha tabia ya kutoa mimba kwani kunahatari kubwa kwa afya zao, huku akiisisitiza jamii kuwaelimisha vijana madhara ya utoaji mimba ili kukabiliana na tatizo hilo ambalo limeshamiri katika sehemu nyingi nchini hasa mijini. 

“Jamii yote ishirikiane na wataalamu wa afya katika kutoa elimu kwa vijana kuepuka tabia ya utoaji mimba ili kuokoa taifa” alisema Dk. Mwako.

MSD yapata suluhisho la DAWA BANDIA

Dar es Salaam. Miezi 10 baada ya kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD), Joseph Mgaya kwa tuhuma za kusambazwa kwa dawa bandia za kupunguza makali ya Ukimwi (ARV’s), uongozi wa bohari hiyo jana umeibuka na kusema kuwa umejipanga kuhakikisha ununuzi wa dawa bandia hautokei tena.
Mbali na kueleza mipango na utendaji wake, bohari hiyo imekiri wazi kuwa, mahitaji ya dawa nchini ni makubwa ikilinganishwa na bajeti inayotolewa na Serikali, kwamba mwaka jana ilihitajika Sh189 bilioni za kununua dawa lakini zilipatikana chini ya Sh100 bilioni.
Imesema tatizo hilo linachangiwa na bajeti finyu, pamoja na uhaba wa viwanda vya kuzalisha dawa nchini, huku ikieleza kuwa kwa sasa kuna viwanda vitatu tu vinavyozalisha dawa nchini. Vingine vikiwa vimefungwa ama kuzalisha dawa za kutibu magonjwa ya aina moja tu.
Akizungumza na Mwananchi mara baada ya kumalizika kwa mkutano wake na wanahabari jana kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, Kaimu Mkurugenzi wa Bohari hiyo, Isaya Mzoro alisema hivi sasa wamekiimarisha Kitengo cha Usimamizi wa Ubora wa dawa na kwamba kinafanya kazi zake vizuri, kwa ukaribu mkubwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).
“Tumekuwa na mikutano kati yetu na TFDA ili kuhakikisha kwamba tunadhibiti ubora wa dawa zinazowafikia Watanzania,” alisema.
Alipoulizwa kwa nini bohari hiyo ilinunua dawa bandia ambazo hazikuwa na ubora unaotakiwa alisema, “Hilo suala sitapenda kulisema hapa kwa sababu linashughulikiwa na vyombo vya sheria, usalama wa taifa na polisi, ila kwa sasa kitengo cha usimamizi na ubora wa dawa kimeimarishwa.”
Oktoba mwaka jana Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi, alimsimamisha kaz
i Mgaya pamoja na maofisa wengine wawili akiwamo Mkuu wa Kitengo na Ofisa wa Idara ya Udhibiti Ubora, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za kusambazwa ARV bandia.
Uamuzi huo ulikwenda sambamba na kufungwa kwa kiwanda kilichotengeneza dawa hizo cha TPI, baada ya kubainika kwa dawa bandia wilayani Tarime.
Dawa hiyo bandia aina ya TT-VIR 30 toleo namba OC.01.85, nyaraka zake zilionyesha kuwa kiwanda cha TPI waliwauzia MSD dawa hiyo iliyotengenezwa Machi, 2011 na kutarajia kwisha muda wa matumizi yake Februari, 2013.
Mzoro alisema mahitaji ya dawa ni makubwa kuliko bajeti ya Serikali na kufafanua kuwa hiyo ndiyo sababu ya maeneo mengine ya nchi kukosa dawa.
“Kwa mfano mwaka jana tulihitaji Sh189 bilioni lakini tulipata fedha chini ya Sh100 bilioni, mwaka huu tunahitaji zaidi ya Sh100 bilioni lakini mpaka sasa fedha tulizonazo ni nusu ya kiwango hicho,” alisema.
Alisema tatizo jingine ni kuwa na viwanda vichache vya kuzalisha dawa nchini na kwamba vilivyopo sasa ni kiwanda cha Shellys, Zenufa na Keko na kwamba viwanda vya Intercane, Tanzasino, TPI na Mansurdaya, ama vimekufa au vinazalisha dawa kwa kiwango kidogo.

Teknolojia: Uingereza sasa yatengeneza nyama ya bandia, huuzwa kwa maelfu ya dola

Uingereza

WATAALAMU wa lishe na maabara wamegundua njia mbadala ya kuzalisha nyama bandia maarufu kama 'burgers' kwa kutumia tishu zinazotoka katika seli za ng'ombe.Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kwa siku kadhaa na kuripotiwa jana na Shirika la Habari la AP ulibainisha kuwa, ingawa utafiti huo uliwagharimu wataalamu zaidi ya Euro 300,000 kuzalisha, wameweza kufikia hatua nzuri

."Lakini hii si burger kama hizi za kawaida inaonesha ni nzuri na watu walijaribu kuionja mjini London, siku ya Jumatatu. Nyama hii iliweza kuzalishwa kupitia maabara kutokana na seli za ng'ombe," ilieleza sehemu ya utafiti huo.

Kwa mujibu wa Mark Post ambaye alikuwa miongoni mwa wataalamu waliongoza timu hiyo kutoka Chuo Kikuu cha Maastricht kilichopo Netherlands ambaye alifanya utafiti huo kwa zaidi ya miaka mitano alisema hayo ni matumaini.
"Ninaamini kuwa kutengeneza nyama kupitia maabara itasaidia kwa hatua kubwa kutatua tatizo la chakula na kupunguza tatizo la uharibifu wa mazingira," alieleza Post katika utafiti huo.
Mbali na hayo, Post alisema kuwa mafanikio hayo hayawezi kuzuia utafiti kuendelea.
"Ili burger hii iweze kufanikiwa katika viwango bora ni lazima ichunguzwe na ikiwezekana kuionja kama kitu cha kawaida," alisema.
Hata hivyo, kwa mujibu wa utafiti huo nyama yao ilitengenezwa kutokana na seli za misuli ya ng'ombe ambayo ilichukuliwa na kuyeyushwa na hatua ya mwisho ikachanganywa na vitu vingine.
"Pia tuliweza kuchanganya chumvi, egg powder, breadcrumbs, red beet juice and saffron," iliongeza utafiti huo.
Aidha, Post na watafiti wenzake kwa mujibu wa utafiti huo walichukua seli za ng'ombe na kuzichanganya katika mpangilio wa lishe ambao uliwasaidia kufikia hatua hiyo ya kutengeneza nyama bandia.

"Muonekano wa ukusanyaji wa seli hizo ulipangiliwa katika chembe ndogo ndogo zaidi ya 20,000 ili kutengeneza gramu 140 za nyama ya burgers," aliongeza Mtafit
 
Support : Copyright © 2013. Tanzania Mpya - All Rights Reserved
Template Modify by Hisia za Mwananchi
Proudly powered by Hisia