Showing posts with label Makala. Show all posts
Showing posts with label Makala. Show all posts

JE, UNADHANI MAVAZI YA NUSU UCHI NI USHAMBA AU MAENDELEO??? Fuatilia mjadala huu makaini hapa

MAVAZI huvaliwa na mtu kwa kusudi la kufunika mwili au sehemu zake na kwa makusudi mengineyo.
Mavazi hukinga mwili dhidi ya baridi au jua kali na athari nyingine zinazoweza kuathiri mwili vibaya.
Kazi nyingine ya mavazi ni kuwasilisha ujumbe kwa watu wengine kwa kuonyesha mtu fulani ni sehemu ya kundi fulani kama vile watoa huduma kwa jamii kama manesi, askari, wachungaji n.k.
Mavazi kwa hakika ni kiashiria cha nje kinachoakisi na kuonyesha taswira ya kile kilichoko ndani ya mtu. Muonekano wa mtu wa nje unatoa picha ya ule wa ndani.

Kumekuwa na tatizo kubwa la wanawake wengi Tanzania na Afrika kwa ujumla kuvaa mavazi yanayoonekana kwa wengi kama ya nusu uchi, yanayobana sana kiasi cha kuchora viungo vyote vya miili ya wavaaji na yale yanayoitwa vimini.
Mavazi nayo yamekuwa kichocheo kikubwa cha watu kutumbukia kwenye vitendo vya ngono, uzinzi, uasherati na kusalitiana kiasi cha kusababisha watu wengi kushindwa kuzuia tamaa za mwili kulingana na kiwango cha ustahimilivu alichonacho mtu.
Nguo fupi na zile zilizobana zimewafanya baadhi ya wanaume kushindwa kujizuia hivyo kuanguka katika matamanio.
Wanawake wameumbwa kwa maumbile tofauti, lakini katika suala la uvaaji, wengi hawajali ni kwa kiasi gani watazua mfadhaiko kwa wanaume.
Hili linadhihirishwa na mwalimu
Frank Molel anayesema: “Kuna maumbile ya mwanamke ambayo mwanaume hatakiwi kuyaona kwa macho ndio maana mabinti wanatakiwa kujisitiri kwa kuvaa mavazi ya heshima. Wanawake wameumbwa kwa umbo zuri ili wawafunulie waume zao uzuri wao na si kuutembeza barabarani.”
Mwalimu Frank anasema kuwa wanawake na mabinti wengi sasa wanavaa nguo zinazoacha sehemu kubwa ya mapaja yakiwa wazi, hali ambayo tofauti na Wazungu huwavutia wanaume na kujawa na tamaa.
Sasa sio jambo la siri kwa wanawake na wasichana wengi kuvaa nguo zinazobana kiasi cha kuchora umbile zima la mwanamke, kitovu wazi.
Mwalimu huyo anasema baadhi ya wanawake na wasichana wanaojua kuwa wamejaliwa maumbile mazuri, huvaa mavazi sio kwa nia ya kujisetili bali kuwavutia wanaume ili washawishike kuingia kwenye vitendo vya ngono na kisha kulaumu kuwa ni tamaa za wanaume bila kujua kuwa chanzo ni wao.
Wako wanawake wanaojidanganya kuwa kuvaa nusu uchi, vimini na nguo za kubana zinazochora miili yao ndio kupendeza jambo ambalo si kweli kiuhalisia wa mambo, kimaadili ya Kitanzania na Kiafrika na hata kinyume na maagizo ya dini.
Utafiti unaonyesha kuwa wanaume wengi wanaopenda kuwaona wanawake na wasichana wakiwa wamevalia vimini na nguo za kubana sio waoaji, bali wanapendelea sana mfumo huu wa mavazi ambao unawasaidia kuchagua yupi wa kumtumia.
Kuna sehemu za maungo ya mawanamke ambazo mwanaume hatakiwi kuziona lakini sasa zimefanywa kuwa za kawaida.
Itakumbukwa kuwa miaka ya nyuma nguo fupi zilipigwa marufuku na baadhi ya wanawake walikamatwa na kufunguliwa mashtaka.
Zipo baadhi ya familia ambazo mama na binti zake wote huvaa vimini. Hakuna wa kumkosoa mwenzake na kumrekebisha. Ukiuliza unaambiwa ‘tunakwenda na wakati’.
Uvaaji wa aina hii umeshazua balaa sehemu kadhaa hapa nchini. Itakumbukwa kuwa katika jiji la Dar es Salaam, kilizuka kikundi cha vijana ambao walikuwa wakiwakamata wasichana na wanawake wanaovaa nguo fupi na kuacha sehemu kubwa ya miili yao wazi, na kuwachania nguo.
Baadhi ya mikoa, vijana hawa wamekuwa wakiwakamata wasichana na kuwabaka.
Katika jiji la Arusha maeneo ya Metropole , vijana waliomshuhudia binti mmoja mrefu aliyekuwa amevalia nguo fupi sana kiasi cha kukaribia kuonekana kwa nguo ya ndani walisikika wakipiga kelele na kumzomea binti huyo huku wengine wakilalamikia hali ile.
“Hivi ni kweli baadhi ya wanawake hawajui thamani yao kiasi cha kuacha maungo yao wazi na kutojisitiri kama inavyotakiwa.”
Je, ni kweli kwamba binti au mama hawezi kupendeza akivaa nguo nzuri zisizobana wala kuacha wazi sehemu kubwa ya mwili wake?
Je, msichana au mwanamke hawezi kuvutia na hivyo kupata mwenzi akiwa kavaa mavazi ya heshima yanayositiri mwili wake?
Je, msichana au mwanamke hawezi kuendelea hadi tu avae ‘vijinguo’ vinavyotakiwa kuvaliwa na mdogo wake au mwanae?
Ni kweli kwamba kila mtindo wa mavazi unaoingia nchini kutoka kwa weupe unafaa kwa wanawake na mabinti wa Afrika?
Kila mtindo wa uvaaji wa nguo sharti ulinde thamani, heshima na hadhi ya mwili wa mwanamke, na sio kuwa kichocheo cha matamanio ya ngono.
“Hata kama heshima ni bure wasipojiheshimu hatutawaheshimu.”
Ni kauli ya mwandishi wa vitabu na makala mashuhuri Richard Mabala katika makala yake inayoelezea umuhimu wa mtu kujiheshimu yeye mwenyewe ndipo astahili kuheshimiwa na wengine.
Maadili yanavyozidi kuporomoka kila siku nani alaumiwe? Wazazi, walezi, watoto, jamii au serikali?
Serikali inapaswa kutunga sheria na sera za kulinda utamaduni wetu wa Kitanzania na Kiafrika ili usiathiriwe na utandawazi ambao tusipoangalia utauzika utamaduni wa Kiafrika endapo tutaacha kuulinda na kuudumisha

TUNAWATAKIA IDDI NJEMA WAISLAM WOTE....... TUKUMBUKE KUIMARISHA AMANI YETU ILIYODUMU MIAKA MINGI. SOTE NI WAMOJA

Leo ni Sikukuu ya Iddi el Fitri. Waislamu nchini wanaungana na wenzao duniani kote kuadhimisha sikukuu hii baada ya kuhitimisha moja ya nguzo kuu tano za Uislamu, kufunga.


Tunachukua fursa hii kuwapongeza Waislamu wote kwa kumaliza salama mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani na leo kusherehekea sikuu ya Iddi el Fitri.

Kwa hapa nchini sherehe za Iddi mwaka huu kitaifa zitafanyika mkoani Tabora ambako Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, atakuwa mgeni rasmi.

Maadhimisho ya sherehe hizo kitaifa yatafanyika katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani humo na pia katika mikoa mingine yote nchini.

Wakati mwezi mtukufu wa Ramadhani ukiwa umefikia tamati, tunapenda kuwasihi Waislamu kuyaendeleza mema yote ya mwezi huo na kujiepusha na uovu na mambo mengine yanayomchukiza Mwenyezi Mungu.

Wakati wa Mwezi wa Ramadhani, tulishuhudia Waislamu katika umoja wao wakihimizana kutenda mambo mema, kusaidia jamii hasa yatima, wajane, watu wasio na uwezo, wagonjwa, kuwa na uvumilivu, subira, kuhimizana mema na kujiweka karibu na Mwenyezi Mungu katika swala na kwa kufuata mafundisho yake.

Katika kipindi hicho, viongozi wa dini wamehimiza upendo, umoja, mshikamano, kuepuka chuki na mambo mengine mabaya na kuufanya mwezi huo kuwa wenye amani, upendo na mshikamano miongoni mwa Waislamu na wasio Waislamu.

Ni matumaini yetu kuwa Mwezi wa Ramadhani hautaondoka na mema yake, bali Waislamu na wasio Waislamu watayaendeleza mema yote waliyokuwa wakiyazingatia katika mwezi huo.

Pia ni matumaini yetu kuwa Waislamu watashirikiana na wenzao wasio Waislamu kusherehekea sikukuu ya Iddi kwa amani na utulivu.


Tunawasihi wananchi kujiepusha na mambo yoyote yanayoweza kuhatarisha usalama wao au wa watu wengine wakati wa kusherehekea sikukuu hii.

Hatutarajii kuona watu wakisherehekea sikukuu hii kwa kujiingiza katika ulevi na mambo mengine maovu yanayoweza kuharibu maana nzima ya sikukuu hii ya kidini.

Aidha, tunatoa tahadhari kwa wazazi kuwa karibu na watoto wao wakati wa sikukuu hizi ili kuwalinda dhidi ya mambo yoyote mabaya yanayoweza kuwatokea. 


Tunasema hivi kutokana na uzoefu kuonyesha kuwa, wakati wa sikukuu za kidini baadhi ya wazazi na walezi wamekuwa wakiwaachia watoto kwenda kutembea katika maeneo mengine ikiwamo katika kundi za starehe na fukwe za bahari bila ya uangalizi ambako mara nyingine hukumbana na masahibu mbalimbali na hata wakati mwingine kupoteza maisha.

Madereva nao tunawaasa kuendesha magari yao kwa tahadhari na kuepeuka kuendesha huku wakiwa wamelewa ili kuepusha ajali zinazoweza kujeruhi au hata kupoteza maisha ya watu watakaokuwa barabarani wakisafiri au katika matukio mbalimbali ya kusherehekea sikukuu.

Pia tunatoa wito kwa Polisi kuimairisha ulinzi kwenye nyumba za ibada ili waumini waswali swala ya Iddi kwa amani na kurejea majumbani.

Tunawatakia Waislamu na Watanzania wote Iddi Mubaraka.

TUNAELEKEA WAPI???

WATANZANIA TUNAELEKEA WAPI? TUNAWAZA NINI?? KWA STYLE HII UMASKINI TUNAPAMBANA NAO VP???
TUBADILIKE.

KATUNI: HII TABIA YA KUWEKA MASLAHI BINAFSI MBELEINAKWAMISHA MAMBO MENGI..........


MALIMWENGU : Ni sahihi kupekua simu ya mwenza wako?

Katika mambo yaliyo magumu kwenye maisha kwa watu walio wengi, basi ni kupekuliwapekuliwa. Wapo wanawake ambao hudiriki hata kuwapekua simu za viganjani  za waume zao na kuweka miaka waliyozaliwa, ili ahakiki mumewe ana shilingi ngapi kwenye akaunti yake ya simu yaani Tigo-pesa, Mpesa au Airtel Money.
Swali la wiki hii liliuliza:
Utakuta mwanamke anapekua simu ya mumewe au mwanaume anapekua ya mkewe, pengine msichana anapekua simu ya mpenzi wake au mvulana anafanya hivyo. Kupekuliana simu ni sawa?
Wadau wa safu hii walijibu hivi:
Prosper Mallya, Moshi
Suala la kupekua simu ya mke wako au mume wako,  mie naona ni suala ambalo limeshakua kama ni mazoea, maana  nyingine ni kama ngozi yako ya mwili hapo ni uaminifu tu unahitajika.
Danny Chumu, Dar es Salaam
Kupekua pekua simu ya mpenzi wako siyo jambo jema hata kidogo inafaa kuaminiana tu wala sioni haja ya kupekua  katika simu ya mwenzi wako.
Ashura Amily, Kibaha
Kupekua simu ya mkeo/mumeo au mpenzi wako ni sawa hapo ndiyo mtaaminiana na mapenzi mliyokuwa nayo ni ya kweli unapata kujua tabia za mwenzi wako.
 
Support : Copyright © 2013. Tanzania Mpya - All Rights Reserved
Template Modify by Hisia za Mwananchi
Proudly powered by Hisia