Showing posts with label Kimataifa. Show all posts
Showing posts with label Kimataifa. Show all posts

CHANJO YA MALARIA YAPATIKANA: Inasemekena, mtu akichanjwa hawezi kuugua tena MALARIA

Wanasayansi nchini Marekani wamesema kuwa wamegundua aina ya chanjo, ambayo mtu akipatiwa hataugua tena ugonjwa wa malaria maisha yake yote.
Ugunduzi huo ambao tayari umefanyiwa majaribio kwa watu kadhaa na kufanya kazi kikamilifu ukiwa pia salama, utaandika historia ya kufuta malaria na kuwa ugonjwa wa nadra kwa watu kuugua.
Taarifa kwa gazeti hili iliyotolewa Alhamisi wiki hii na Taasisi ya Marekani ya Kudhibiti Magonjwa ya Kuambukiza na Mzio (NIAID), inaeleza kuwa chanjo hiyo iliyopewa jina, PfSPZ imeonyesha mafanikio hayo kwenye hatua yake ya awali ya majaribio.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mtu akipatiwa chanjo hiyo mwili wake unatengeneza chembe kinga ambazo zinakuwa na uwezo wa kuangamiza vimelea wa malaria katika hatua yake ya mwanzo mara baada ya kuumwa na mbu.
Chanjo ya PfSPZ, inaelezewa kutengenezwa kwa vimelea dhaifu wa malaria ambao huhamasisha mwili kutengeneza askari wa kudumu.
Kumbukumbu za Shirika la Afya Duniani (WHO) za mwaka 2010, zinaonyesha kuwa zaidi ya watu 3.3 bilioni, ambao ni karibu sawa na nusu ya dunia nzima wapo kwenye hatari ya kuugua ugonjwa wa malaria.
Katika kipindi cha mwaka huo, inaripotiwa kuwa watu 210 milioni walibaini kuugua malaria, baada ya kupimwa hospitalini ambapo takriban 660,000 walipoteza maisha.
Asilimia 90 ya waliopoteza maisha walikuwa kutoka Bara la Afrika, licha ya juhudi kubwa za kusambaza vyandarua vyenye dawa na dawa za tiba.
WHO inasema kuwa kuongezeka kwa mbinu za kuzuia na kutibu malaria katika maeneo mbalimbali duniani kumesaidia kupunguza tatizo la malaria kwa asilimia 25 na kwa asilimia 33 katika Bara la Afrika.
Imesema kuwa nchi nyingi za Afrika zina uwezo mdogo wa kifedha, hivyo hutegemea mataifa tajiri kuzisaidia kwa kuwezesha kupatikana vifaa vya kuzuia malaria na dawa za tiba za bei nafuu, hata kutolewa bure kwa watoto na wajawazito.

Hatimaye Rais Kagame wa Rwanda Amjibu KIKWETE.... Asisitiza, hawezi kuongea na waasi....

Serikali ya Rwanda imetoa tamko linaloonyesha kutoielewa kauli ya Rais Jakaya Kikwete, iliyoamuru wahamiaji haramu kuondoka nchini, hali inayoonekana kukwepesha hoja.
Rwanda kupitia waziri wake wa Mambo ya Nje, Louise Mushikiwabo, ilikaririwa ikieleza kwamba hawatajibu mapigo agizo la Rais Jakaya Kikwete ya kuwataka Wanyarwanda wote waliolowea Magharibi mwa Tanzania kuondoka haraka.
Mushikiwabo alisema wako tayari kuwapokea na kuwalinda wote waliofukuzwa Tanzania kwa kisingizio kuwa ni wahamiaji haramu, akieleza kwamba anasikitishwa kwa kuwa Tanzania haikufanya jitihada yoyote kuwasiliana na Rwanda kuhusu suala hilo kabla ya kuchukua uamuzi huo.
“Ni uamuzi ambao umeshachukuliwa, hatukushirikishwa kwa namna yoyote na jukumu letu kama serikali na taifa ni kuwahakikishia ulinzi wote wanaokuja, na hili ndilo suala tunalolishughulikia kwa sasa,” alisema.
Kwa mujibu wa gazeti la New Times, Mushikiwabo aliwaeleza waandishi wa habari kwamba agizo hilo la Rais Kikwete pamoja na ushauri wa kuitaka Serikali ya Rwanda kuzungumza na wanamgambo hasimu wa FDLR waliopo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), hayatayumbisha uhusiano imara baina ya Watanzania na Wanyarwanda.
“Sisi si majirani tu, tuna mfungamano imara baina ya watu wetu pia, tuna mfungamano wa damu, wa kibiashara, na mengine mengi ya kutufanya tuendelee kuwa pamoja,” alisema na kutumia fursa hiyo kuwakaribisha Watanzania nchini Rwanda.
Watanzania wanaweza kuishi hapa kwa umri wowote wanaotaka. Tunawachukulia kuwa ni watu wetu muhimu kwenye fungamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki,” alisisitiza.
Rais Kikwete wakati akihitimisha ziara yake mkoani Kagera alitoa agizo la kuwataka wanaomiliki silaha kinyume cha sheria na wahamiaji haramu ama kuondoka au kuhalalisha ukazi wao, huku akitoa wiki mbili kwa zoezi hilo kutekelezwa, kabla ya kuanza kwa operesheni ya kuwasaka watu hao.
Kauli hiyo ilitokana na kushamiri vitendo vya kihalifu katika eneo la Kanda ya Ziwa, Rais hakutaja jina la nchi ya wahamiaji hao. Kwa ukanda huo Tanzania inapakana na Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na DRC.
Pia, Rais Kikwete katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi alizungumzia kusikitishwa na kauli za shutuma, kejeli na udhalilishaji zilizotolewa na Rais Paul Kagame wa Rwanda dhidi yake.
Mvutano baina ya Rwanda na Tanzania ulianza kuwekwa hadharani Mei mwaka huu, baada ya Rais Kikwete kuishauri Rwanda kukaa na kuzungumza na FDLR wenye makao yao DRC, hatua ambayo haikuifurahisha Serikali ya Rwanda.
Wakati Rwanda ikieleza hayo jana Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue alizungumza na gazeti hili, na kutaka majibu ya kauli hiyo ya Rwanda yatolewe na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiao wa kimataifa
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Mkumbwa Ally alisema kauli iliyotolewa na Rais Kikwete ilikuwa ni ushauri, kwamba Rwanda wanaweza kuukubali ama la.
“Kilichomkasirisha Rais Kikwete ni lugha za matusi zilizokuwa zikitolewa na viongozi wa Rwanda, ila kwa hicho walichokisema sidhani kama kitakuwa na tatizo kwetu,” alisema Mkumb
wa.
Alifafanua kwamba, alipokuwa mkoani Kagera Rais Kikwete hakutoa agizo la Wanyarwanda kufukuzwa, bali alitoa agizo la kuanza kwa operesheni ya kuwakamata wahamiaji haramu, wale wanaomiliki silaha kinyume na taratibu.
“Rais alizungumzia masuala ya jinai ‘Criminal Element’, siyo kuwafukuza Wanyarwanda,” alisisitiza.
Hatutazungumza na FDLR
Waziri wa Mambo ya Nje, Louise Mushikiwabo, aliendelea kusema sera ya Rwanda kuhusiana na makundi ya aina hiyo, iko wazi na haitabadilika, kauli ambayo amekuwa akiirudia kila mara na kuwataka wote wanaofikiria kuhusu Rwanda kuzungumza na FDLR kwa namna yoyote kusahau wazo hilo.
“Kama umehusika kwa namna yoyote na maangamizi, wewe utakuwa adui wa kila mtu. Ni wazi kwamba Wanyarwanda wote watakuwa kwenye majonzi iwapo kwa namna yoyote kutakuwa na mawasiliano ya FDLR,” alifafanua.
Kundi la FDLR ambalo ni kifupisho cha Democratic Forces for the Liberation of Rwanda, linaundwa na watu walioshiriki kwenye mauaji ya kimbari yaliyowalenga watu wa kabila la Watutsi mwaka 1994, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 800,000 kwa miezi mitatu.
Kundi hilo ambalo limeweka makazi yake mashariki mwa DRC, linadaiwa kufanya mashambulizi kadhaa yakiwamo ya milipuko ya mabomu nchini Rwanda, ambapo mwezi uliopita shambulio la aina hiyo mjini Kigali lilisababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi watu kadhaa.
Uhusiano wa kihistoria
Familia za Rwanda zikiwamo zilizoishi Tanzania tangu miaka ya 1950, zimeelezwa kuwa zimekuwa zikiwasili nchini humo kupitia mpaka wa Rusumo baada ya agizo la Rais Kikwete kuwataka wawe wameondoka ndani ya wiki mbili, kabla ya kuanza kwa operesheni rasmi ya kuwaondoa.
Kwa mujibu wa mamlaka nchini Rwanda, mamia ya Wanyarwanda waliokuwa wakiishi mkoani Kagera ambako ndiko Tanzania inapopakana na Rwanda wamekuwa wakirejea kwa wingi, ambapo hadi juzi, zaidi ya watu 300 walikuwa wameshaorodheshwa kwenye ofisi za Uhamiaji.

PAPA FRANCIS Atoa salamu za IDDI, Awatakia waislam wote iddi njema ahimiza ushirikiano na kuheshimiana kati ya waislam na wakristo

Papa Francis, amewatakia Waislamu wote duniani, sikukuu njema ya Eid el- Fitr huku akiwahimiza kuheshimiana zaidi kupitia elimu.
“Mwaka huu wa kwanza kama kiongozi wa Kanisa Katoliki, nimeamua kutuma ujumbe huu kwenu marafiki zangu Waislamu nikiwa na heshima kubwa. Ninatambua uhusiano, udugu na urafiki baina yetu sisi,” alisema Papa Francis katika salamu zake.
Makao ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani, yameulezea waraka huo kuwa ni wa salamu maalumu za Sikukuu ya Eid al-Fitr inayofanyika duniani leo, baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
“Ujumbe wangu katika mwaka huu ni kuwataka nyote kuakisi kwa pamoja matendo yetu ya kiimani kama Waislamu na Wakristo na kukuza ushirikiano na kuheshimiana,” alisema Papa Francis.
Ameongeza: “Kuhusu elimu kwa waumini wetu vijana wa Kiislamu na Kikristo, hatuna budi kuwalea na kuwakuza wakifikiri na kuzungumzia namna nzuri ya kuheshimiana katika imani za wenzao na waumini wao na kuepuka tabia ya kudharau au kubeza imani na mafundisho ya wengine.”
Kwa kawaida salamu hizo hutolewa na Vatican kupitia Baraza la Kipapa la Mijadala ya Kiimani, lakini safari hii Papa Francis ameamua kutuma salamu hizo mwenyewe tangu alipofanya hivyo Papa Yohane Paul II mwaka 1991.
Papa Francis aliendelea kueleza, “Kuhusu kitu gani tunatakiwa kuheshimana kama binadamu ni maisha, utu wa mtu na kupatikana kwa heshima na haki ya mtu.”
Papa Francis alisema watu wa imani mbili tofauti hawana budi kuheshimiana.
Ili kufikia azma hiyo familia, shule, mafundisho ya kidini na aina zote za vyombo vya habari vina wajibu wa kushiriki.
“Tunafahamu kuwa heshima ya mtu ni ya msingi katika uhusiano wowote wa binadamu, hasa kati ya watu ambao wanakiri imani za kidini. Kwa maana hii, kwa moyo wa dhati, tutakuza urafiki wetu.”
Kiongozi huyo wa waumini bilioni 1.2 duniani alisema kutakiana mema wakati wa sikukuu ni kuheshimiana, ingawa si kukubaliana kwa kila jambo linalofanyika kwenye imani nyingine.
“Tunashiriki nao katika furaha, hatuzungumzii imani na mioyo yao,” alisema.

OMEGA: Hoteli yabainika kuuza nyama za watu, watu washangaa, yabomolewa

Polisi walifanikiwa kuvikamata vichwa hivyo baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema wanaoishi karibu na hoteli hiyo ambapo mbali na vichwa hivyo viwili lakini pia walikamata bunduki mbili aina ya  AK47,kofia mbili za jeshi pamoja na simu nyingi.

Watu saba wanashikiliwa na jeshi la polisi nchini Nigeria katika hoteli moja iliyopo karibu na soko moja maarufu sana nchini humo linalofahamika kwa jina la Ose-Okwodu katika mji wa Anambra baada ya kukamatwa kwa vichwa viwili vya binadamu vikiwa bado vibichi lakini jina la hoteli hiyo linahifadhiwakutokana na sababu za kiusalama
hotel human heads in onitsha 
“kila wakati nimekuwa nakuja hapa sokoni na kufanya biashara zangu katika hoteli hii kwasababu ipo karibu sana na soko.lakini nilikuja kugundua mambo ambayo sio ya kawaida ikiwemo watu wakiingia na kutoka katika hoteli hii,chakushangaza zaidi ni kutokana na watu hao kuwa ni wachafu sana wakati mwingine wakiwa wamechafuka damu,kwahiyo sikushangaa sana kusikia polisi wamegundua unyama huo jan
a asubuhi”alisema jamaa mmoja muuza mboga mboga katika eneo hilo.




Mchungaji mmoja ambaye ni mmoja kati ya watu waliowatonya askari kuhusu biashara hiyo ya nyama za watu katika hoteli hiyo alisema "niliwahi kwenda kwenye hoteli hiyo mapema mwaka huu,niliagiza chakula lakini baada ya kula nilihisi nyama ilikuwa na chumvi kwa kiwango cha N700,nilishangaa sana.kwahiyo sikujua kama ni nyama ya binadamu au la nilishangaa kwasababu ilikuwa inauzwa ghali sana”alimalizia mchungaji huyo



SOURCE: DJ SEK BLOG

MSHANGAO: Ndugu watano wafunga ndoa siku moja

Nakuru. Katika hali isiyo ya kawaida wanandugu watano kutoka familia moja wamefunga ndoa siku moja nchini Kenya.
Tukio hilo lililoibua mshangao  miongoni mwa watu walioshuhudia lilitokea katika kanisa la mtakatifu Peter mjini Nakuru.
Maharusi waliojawa na furaha isiyo na kifani walielezea kuwa malezi yao bora yaliwafanya wote  kuchagua kufunga ndoa siku moja.
Samson Wachira, ambaye ni wa kwanza kuzaliwa alisema wazazi wao waliwaonyesha kupendana na kushirikiana katika mambo yote tangu wakiwa wadogo hali iliyowapelekea kukua katika mazingira hayo.
Hivyo basi, Wachira alielezea kuwa kila mmoja wao alipotaka kufunga ndoa rasmi, aliwaita nduguze kwa ushauri.
Wachira ana mika 36 ilhali George Wango, ambaye ni wa mwisho kuzaliwa  ana umri wa miaka 24.
Wengine walikuwa Peter Mbugua, 35, Stephen Kinyanjui, 34, na Harman Kago,32.
Ndugu hao waliitaja siku hiyo kama ya furaha ambayo walikuwa wakiingojea kwa hamu kubwa kutokana na kufikia kupiga hatua moja maishani mwao .
“Tumekuwa tukiingoja
na kujitayarisha kwa siku hii kwa mwezi mmoja uliopita,” alisema Wango, mmoja wa maharusi hao
Wazo la kufunga ndoa siku moja liliwajia ndugu hao miezi saba iliyopita wakati kasisi mmoja alipowatembelea nyumbani kwao  eneo la Kiratina.
Baba yao aliandaa karamu na ibada ya misa ya shukrani wakati kasisi alitaka kujua ni nani kwa familia hiyo alikuwa amekubaliwa kupokea sakramenti.
Kulingana na desturi za kanisa la Katoliki, ni sharti mwanamume awe amefunga ndoa rasmi kanisani ili kuruhusiwa kupokea sakramenti hivyo kasisi huyo aliwapa changamoto vijana hao kuhusu faida za kufunga ndoa kanisani.
Baada ya kushauriana baina yao, vijana hao walienda kuomba mawaidha kutoka kwa baba yao James Kago ambaye aliwapa moyo na kuwahamasisha kufunga ndoa siku moja.
 “Niliwahimiza wafunge ndoa siku moja kwani hii ingewawezesha kufanya haraka, kupunguza gharama na zaidi ya hayo kuwaunganisha,” alisema Kago
Kwa mwezi mzima uliopita, familia ya Kago  ilikua  ikizunguka kwa wazazi wa wakwe zao watarajiwa  mmoja baada ya mwingine ili kupeleka mahari na kuomba idhini ya kufunga ndoa rasmi.

Kinyume na wengi, wanawake waliokuwa wakiolewa walimsifu sana mama mkwe hasa kwa kuunga mkono ndoa hizo na kuwashauri.

Mgogoro wa DRC vs M23: MAREKANI ""RAIS KAGAME NA RWANDA WANAHUSIKA'''


Marekani yaitaka Rwanda kusitisha mara moja misaada ya kijeshi kwa waasi wa M23 nchini Congo.  Uchunguzi wa UN umepata ushahidi wa wazi kuwa Serikali ya Rais Kagame imekuwa ikitoa msaada wa kijeshi kwa waasi nchini Congo.


A M23 rebel trainer walks behind recruits during a training session at the Rumangabo military camp in eastern Democratic Republic of Congo, May 16, 2013.




NIGERIA: Bikira Maria asadikiwa kuonekana huko Nigeria na kuwafanya watu kuvutwa na tukio hilo


                                                                                                                                             
Mmoja kati ya mashuhuda

Picha hii ni ya Kanisa la Kikatoliki la Saint Benedict, lililopo Ubiaja, Esan Kusini Mashariki ya Jimbo la Edo nchini Nigeria.


Waumini wa Kanisa hilo wanasema kwamba waliiona kitu kinachofanana na Bikira Maria kwenye ukuta wa Kanisa hilo mnamo siku ya Jumapili July 21.

Siku ya vijana wakatoliki Duniani: POLISI YAGUNDUA KUWEPO KWA BOMU wakati maelfu walipojitokeza kumpokea Baba mtakatifu Francis

Baba Mtakatifu Francis amelakiwa na maelfu ya mahujaji wa Brazil wakati akianza ziara yake ya kwanza ya nje tangu achaguliwe kuwa mkuu wa Kanisa Katoliki.
Baba Mtakatifu huyo wa kwanza kutoka Amerika ya Kusini alitembelea jiji la Rio De Janeiro, akiwa kwenye gari la wazi na kisha kukutana na Rais Dilma Rousseff , katika kasri la taifa la gavana. Yuko Brazil kuhudhuria Sherehe za Siku ya Vijana Wakatoliki Duniani.Baada ya kuondoka, polisi walifyatua mabomu ya kutoa machozi, kuwatawanya waandamanaji wanaoipinga serikali na gharama kubwa za ziara hiyo.
Katika hotuba yake mara baada ya kuwasili, Baba Mtakatifu alitoa wito kwa vijana Wakatoliki kuwa manabii wa mataifa yote.
“Nimekuja kukutana na vijana kutoka sehemu zote duniani, waliovutika kwenye mikono ya Yesu Kristo Mwokozi,” amesema akiimanisha sanamu maarufu ya Yesu iliyopo katika jiji la Rio.
“Wanataka kutafuta hifadhi katika mikono yake, karibu kabisa na moyo wake ili wasikie wito wake kwa nguvu na wazi.”
Takriban saa moja mara baada ya sherehe za kumkaribisha, polisi walifyatua mabomu ya kutoa machozi na yale ya kushtua dhidi ya waandamanaji nje ya kasri.
Yalikuwa ni maandamano ya hivi karibuni ambayo waandamanaji wanasema ni ya kupinga vitendo vilivyokithri vya rushwa ndani ya serikali na nchi nzima.
Lakini baadhi yao wamechukizwa na dola za Kimarekani milioni 53 zilizotumika kuandaa ziara ya Baba Mtakatifu.

Kulikuwa na uharibifu kiasi na watu kadhaa kukamatwa, lakini ilikuwa kama ishara kwamba, upo uwezekano wa ziara hiyo ya kihistoria ya Baba Mtakatifu ikagubikwa na matukio yasiyo ya kawaida ya kisiasa.
Katika hatua nyingine, jeshi la Brazil limesema, bomu la kutengeneza nyumbani limegunduliwa karibu na eneo moja takatifu kati ya Rio na Sao Paulo ambalo kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki anatarajiwa kulitembelea siku ya Jumatano.
Bomu hilo lilikowa na nguvu kidogo, lilidhibitiwa baadaye.

Wakati Baba Mtakatifu Francis akiteremka kutoka kwenye ndege ya shirika la Alitalia, kwenye uwanja wa ndege wa Rio, mapema Jumatatu, alilakiwa na Rais Rousseff huku umati wa watu ukishangilia na alikabidhiwa shada la maua, huku kwaya ya vijana ikiimba wimbo unaohusu siku ya vijana.
Aliwapungia mkono watu na msafara wake kuelekea katikati ya Rio ambako maelfu ya mahujaji walikuwa wamekusanyika.
Baba Mtakatifu Francis alionekana mwenye furaha na kutulia wakati akielekea jijini Rio akiwa ndani ya gari la kawaida huku dirisha likiwa limefunguliwa na maafisa usalama wakihangaika kuudhibiti umati.

Kulikuwa na matukio ya fujo wakati gari lake lilipokwama kwenye moja ya msongamano wa magari katika jiji la Rio, baada ya dereva wake kukosea njia na kuzikosa zile zilioandaliwa kwa ajili ya msafara wa Papa.

Mara umati ulizingira gari lake ukiwa na matumaini ya kumuona kwa karibu ama kumgusa. Mwanamke mmoja alimpitisha mtoto wake kwenye dirisha la gari ili Baba Mtakatifu ambusu.
Alipofika katikati ya jiji Papa alipanda gari la wazi lililoandaliwa maalum kwa ajili yake, huku akipunga mkono kwa maelfu ya watu waliojipanga pembezoni mwa barabara.
“Siwezi kusafiri kwenda Rome, lakini amekuja kuifanya nchi yangu kuwa njema na kuimarisha imani yetu,” alisema mzee mmoja wa miaka 73, Idaclea Rangel, huku akibubujikwa na machozi.
Mamlaka imeimarisha ulinzi wakati wa ziara ya siku saba ya Papa, kufuatia wiki kadhaa za maandamano nchi nzima kupinga rushwa na utawala mbovu.
Papa Francis alikataa kutumia gari maalum lisilopenyeza risasi, licha ya maombi kutoka kwa maafisa wa Brazil, maafisa wa usalama wapatao 30,000, jeshi na polisi wataimarisha ulinzi wakati wa ziara hiyo.
Zaidi ya vijana Wakatoliki milioni moja wanatarajiwa kukusanyika Rio kwa ajili ya Siku ya Vijana Duniani, ambyo huadhimishwa kila baada ya miaka miwili, ni sherehe za waumini Wakatoliki.

Papa huyo mzaliwa wa Argentina, ambaye alishika wadhifa huo Machi mwaka huu, anatarajiwa kuongoza ibada katika ufukwe wa pwani ya Copacabana siku ya Alhamisi na pia kutembelea moja ya vitongoji masikini.

ROYAL BABY BUZZ?? Kate Middleton and Prince William Welcome Royal Baby ... It's a Boy!

It's a prince! On Monday, the world welcomed the newest addition to the royal family and the future heir to England's throne. Palace officials confirmed the arrival of His Royal Highness the Prince of Cambridge, born at St. Mary's Hospital at 4:24 PM BST, and weighing 8 lbs 6 oz..

"Her Royal Highness and her child are both doing well and will remain in hospital overnight," palace officials stated in an official press release. Prince William was present at the birth of his first child. The name of his firstborn son will be released "in due course."

"The Queen, The Duke of Edinburgh, The Prince of Wales, The Duchess of Cornwall, Prince Harry and members of both families have been informed and are delighted with the news," according to the brief statement emailed to members of the press, many of whom have been camped outside of St. Marys Hospital for days. 

Prince Charles expounded on the emotional moment in history, in a statement released through Clarence House. He said he is "enormously proud and happy to be a grandfather for the first time."

"Both my wife and I are overjoyed at the arrival of my first grandchild," he added. "It is an incredibly special moment for William and Catherine and we are so thrilled for them on the birth of their baby boy."
The birth marks a new era for not only the first-time parents but also the extended royal family. As third in line to succeed the throne after his grandfather Prince Charles and his father, Prince William, he's the first baby born under new succession laws.
 
Support : Copyright © 2013. Tanzania Mpya - All Rights Reserved
Template Modify by Hisia za Mwananchi
Proudly powered by Hisia