Home » » SAKATA LA DAWA ZA KULEVYA NCHINI: VIGOGO, MAWAZ

SAKATA LA DAWA ZA KULEVYA NCHINI: VIGOGO, MAWAZ

Siku chache baada ya kijana mmoja wa Kitanzania aliyeko gerezani mjini Hong kong nchini China kuandika waraka akielezea sababu za yeye kujihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya na kuwataja baadhi ya vigogo wa dawa hizo nchini, hali imeendelea kuwa tete baada ya mawaziri wawili kuhusishwa katika biashara hiyo. 

Mbali na mawaziri hao wawili (majina tunayo) pia wabunge watatu wa viti maalumu wakiwemo wachungaji wakubwa hapa nchini (majina yanahifadhiwa) nao wamedaiwa kuhusika na biashara hiyo huku wakitumia vitambulisho vya Ikulu ili kufanikisha kazi zao.
Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki katika mhadhara wa kongamano la kidini kwenye Ukumbi wa Kanisa la TAG Uyole jijini Mbeya na wanafunzi wawili ambao walikuwa wanafanya biashara hiyo (majina tunayo) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na St. Gasper cha Morogoro wakati wakisalimisha kilo tano za heroine.
Dawa ambazo walikuwa wakizisambaza jijini Mbeya ambapo baada ya kuguswa na neno la Mungu waliamua kuzisalimisha mbele ya kanisa hilo.
Wakizungumza katika kongamano hilo vijana hao walisema kuwa, kwa muda mrefu wamekuwa wakitumiwa kusafirisha dawa za kulevya katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi hali ambayo imekuwa ikiwanufaisha vigogo wa dawa za kulevya ilhali wao wakiishia magerezani.


Sababu za kusalimisha

“Tumeamua kujisalimisha mbele ya Mungu, tumeamua kuzisalimisha dawa hizi mbele ya Mungu, tunatubu kwa dhambi tulizozifanya, tumeiangamiza jamii isiyo na hatia...tunatubu mbele ya Mungu,” alisema mmoja wa vijana hao (jina tunalo) huku akibubujikwa na machozi mbele ya umati wa waumini waliohudhuria kongamano hilo.
Akitoa ushuhuda mbele ya ya waumini waliokuwa katika kongamano hilo ambalo liliongozwa na wachungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kipentekoste, William Mwamalanga na Mchungaji Daud Mwalonde wa Kanisa la TAG Calvary Tempo, mmoja wa vijana hao alisema kuwa amekuwa katika biashara hiyo kwa zaidi ya miaka sita ambapo amesafiri katika nchi mbalimbali za Asia kama vile Afghanistan, India na nchi kadhaa za Bara la Afrika.
Alisema kuwa, huko walichukua na kuzisafirisha dawa hizo na kupata ujira mdogo ambao haukuweza kukidhi mahitaji yao ya kila siku hivyo wameamua kujisalimisha kwa kuwa wanaamini kuwa maisha ya hapa duniani wameshindwa kufanikiwa na mbele ya Mungu wataingia motoni.
Alisema kuwa, yeye pamoja na mwenzake walikuwa wamesimama Uyole wakitokea jijini Dar es Salaam kwa mtu mmoja waliyemtambulisha (jina linahifadhiwa) ambako ndiko hufanya kituo kabla ya kusambaza mzigo huo katika vituo vya mipaka ya Tunduma hasa Wilaya ya Momba na Kasumulu Kyela ambako mzigo husafirisha nje ya nchi.


 Mawaziri wamo  

   Alibainisha kuwa, katika biashara hiyo wamo mawaziri wawili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano nchini akiwemo mmoja anayehusishwa na ugombea urais mwaka 2015 na Naibu Waziri katika moja ya Wizara za serikali ya Jamhuri ya Muungano (majina tunayo). Aidha, kijana huyo alisema kuwa mtandao huu wa dawa za kulevya pia unawahusisha baadhi ya wachungaji maarufu nchini (majina tunayo) ambao alidai wanapokuwa katika biashara hiyo hutumia vitambulisho vya Ikulu na kufanikiwa kupenya maeneo mbalimbali nyeti ili kufanikiwa kupitisha dawa za kulevya.Akiendelea kutoa, ushuhuda katika kongamano hilo ambalo lililenga kuombea amani na utulivu wa nchi, alisema kuwa baadhi ya klabu za kusaidia watoto wagonjwa wanaosafirishwa kwa ajili ya matibabu nje ya nchi pia zinahusishwa katika usafirishaji wa dawa za kulevya. 



 Aliwataja  baadhi ya wabunge watatu wa viti maalumu na wabunge wastaafu kutoka chama tawala (majina yanahifadhiwa) ambao humiliki maduka makubwa katika majiji ya Dar es Salaam, Mbeya, Tanga, Arusha, Dodoma, Mwanza na baadhi ya nchi za Kiarabu ambapo walidaiwa huwa wanawatumia baadhi ya wasanii na waimbaji wa nyimbo za Bongo fleva zikiwemo za Injili katika usambazaji wa dawa hizo kwa mashabiki.Mara baada ya kusalimisha dawa hizo aina ya heroine, Mchungaji Mwamalanga aliamuru dawa hizo zichomwe moto na kutumbukizwa katika shimo la choo ambapo vijana hao baadaye viongozi wa dini waliwahifadhi.

   Akizungumza sababu za kuzichoma moto na kuzitunbukiza katika shimo la choo badala ya kuzisalimisha kwa Tume Inayohusika na Uratibu wa Dawa za Kulevya nchini ili kuzihakiki, Mchungaji Mwamalanga alisema kuwa waliamua kufanya hivyo baada ya kuona kuwa dawa hizo zimekuwa zikirejea mikononi mwa watumiaji baada ya kukamatwa.Alisema kuwa, kulingana na taarifa walizonazo ni kwamba mara kadhaa watuhumiwa wa dawa za kulevya hukamatwa lakini dawa hizo zimekuwa zikirudi kwa watumiaji na kufanya jitihada za mapambano dhidi ya dawa za kulevya kugonga mwamba.
Akizungumza na Majira Dar es Salaam jana, Bw. Rage alisema Mbunge yeyote hawezi kushtakiwa mahakamani anapotekeleza wajibu wake ndani ya Bunge hivyo kituo hicho kinapaswa kuwaacha wabunge na viongozi wa Serikali wafanye kazi zao bila vitisho.
Alisema, kabla kituo hicho hakijafikia uamuzi huo, kinapaswa kupitia Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge namba tatu pamoja na Katiba ya nchi Ibara ya 100 ili kujiridhisha kama kuna uhalali wa kumfungulia mashtaka Bw. Pinda.
“Kama LHRC wamekerwa na matamshi ya Waziri Mkuu aliyoyatoa bungeni mjini Dodoma kwa niaba ya Serikali, waende kulalamika kwa Spika wa Bunge si kumfungilia mashtaka kwa kigezo cha kuangalia haki.
“Tusiangalie haki peke yake bila wajibu, suala hili linakuzwa kwa shinikizo la kisiasa jambo ambalo halipaswi kushabikiwa hata kidogo, mtu yeyote ambaye atakataa kutii amri halali, polisi anaruhusiwa kutumia nguvu ya ziada,” alisema.
Bw. Rage alikwenda mbali zaidi na kuongeza kuwa, yupo tayari kumsaidia Bw. Pinda akishirikiana na wabunge wenzake wa CCM ambao wanamuunga mkono kwa kuhakikisha kama Waziri Mkuu atafikishwa mahakamani, watasimamisha wanasheria makini wa kumtetea na kushinda.
“Kama leo hii tutaruhusu LHRC imfungulie mashtaka Waziri Mkuu bila sababu za msingi mbali ya kulinda sheria za nchi, upo uwezekano mkubwa wa wabunge wengine kufanyiwa kitendo kama hicho...mbunge anapozungumza ndani ya Bunge haruhusiwi kushtakiwa kwa kauli yake,” alisema Bw. Rage.
Aliongeza kuwa, Jeshi la Polisi nchini lina kaulimbiu inayosema ‘Utii wa Sheria bila Shuruti’, hivyo watu wote wanaokataa kutii amri halali wanatambua madhara yanayoweza kutokana na ukiukwaji huo hivyo alichosema Bw. Pinda ni sahihi.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Mkurugenzi wa Uboreshaji na Utetezi kutoka LHRC, Bw. Harold Sungusia, alisema wanakamilisha taratibu za kufungua mashtaka dhidi ya Bw. Pinda katika Makahama Kuu.
Alisema Bw. Pinda amevunja katiba ya nchi kwa kusema kuwa, “Ukifanya fujo na umeambiwa usifanye hiki na wewe ukaamua kukahidi utapigwa tu, maana hakuna namna nyingine...ehee wote tukubaliane kuwa nchi inaongozwa kwa misingi ya kisheria sasa kama wewe ukijifanya jeuri utapigwa tu.
“Na miminasema muwapige tu kwasababu hakuna namna nyingine maana tumechoka”, alisema Bw. Pinda ambapo Bw. Sungusia aliongeza kuwa, kauli hiyo ni kinyume na Katiba, Sheria za nchi na misingi ya Haki za Binadamu.


Bw. Sungusia aliongeza kuwa, kituo hicho kilitegemea Bw. Pinda angefuta kauli yake ambayo aliitoa katika Bunge la Bajeti lililoisha hivi karibuni lakini hadi sasa hajafanya hivyo.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan Tanzania Mpya untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Hisia za Mwananchi

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2013. Tanzania Mpya - All Rights Reserved
Template Modify by Hisia za Mwananchi
Proudly powered by Hisia