Home » » SHEHE achomwa kisu wakati akiendesha IBADA YA EID Mbeya, atuhumiwa kufuga Nguruwe

SHEHE achomwa kisu wakati akiendesha IBADA YA EID Mbeya, atuhumiwa kufuga Nguruwe

Ibada ya Sikukuu ya Eid El Fitr jana iligeuka kuwa uwanja wa mapambano wilayani Kyela mkoani Mbeya, baada ya kutokea vurugu za kushambuliana kwa kuchomana visu na kusababisha watu watatu kujeruhiwa.

Kati ya wali
ojeruhiwa ni Sheikh wa Wilaya ya Kyela, Nuhu Mwafulango, ambaye anatuhumiwa na baadhi ya waumini kuwa pamoja na mambo mengine anajihusisha na ufugaji wa nguruwe.


Tukio hilo lilitokea saa 2:30 asubuhi katika Msikiti mkuu wa wilaya, karibu na Hospitali ya Wilaya ya Kyela, wakati Sheikh huyo akiendelea kusalisha waumini waliohudhuria ibada hiyo.

Waliojeruhiwa katika vurugu hizo, ni Khamis Husein ambaye amechomwa kisu kichwani  wakati akijaribu kumuokoa Sheikh aliyekuwa akiendelea kushambuliwa na waumini hao.

Wengine waliojeruhiwa wamefahamika kwa jina moja moja ni Dk. Magogo na Ustadhi Issa, ambao wote wamepelekwa katika hospitali ya wilaya ya Kyela kwa matibabu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman, alithibitisha kutokea kwa ghasia hizo na kwamba watu sita ambao wanadaiwa kuwa chanzo cha vurugu hizo wamekamatwa na wanahojiwa katika kituo kikuu cha polisi Kyela.

Kamanda Athumani alisema anasubiri taarifa kutoka kwa maofisa wa polisi Kyela kuhusu tukio zima la vurugu hizo na kwamba taarifa alizopata, vurugu hizo zimetulia na waumini wamerejea kuendelea na ibada kama kawaida.

Kamanda  Athmani amewataja waliokamatwa kuhusiana na vurugu hizo kuwa ni  Mashaka Khasim(30), Issa Juma(37), Ahmed Khasimu(35), Ibrahim Shaban (17) Shaban (17), Ambokile Mwangosi(19) na Sadick Abdul(28)Sheikh Mwafungo, akizungumza na NIPASHE kwa simu akiwa katika kituo cha polisi Kyela kwa ajili ya kuchukua fomu ya matibabu (PF3), alisema alivamiwa na waumini wa msikiti huo wakati akiswalisha na kuanza kumshambulia kwa marungu katika sehemu kadhaa za mwili wake.

“Wakati nimeinama chini kupiga sigida kuongoza ibada ghafla nikavamiwa na baadhi ya waumini ambao walinishambulia kwa marungu na hadi sasa nimejeruhiwa mguu, shingo, mkono na goti,” alisema Sheikh Mwafungo.

Alisema sababu kubwa ni kwamba wapo baadhi ya waumini wa msikiti huo ambao wanahitaji madaraka katika msikiti huo na hivyo wamekuwa wakimzushia mambo mengi na kupinga Baraza la Waislamu Wilaya ya Kyela (Bakwata) kutokana na sababu zao binafsi.

Sheikh Mwafulango, alisema baadhi ya mambo ambayo wamekuwa wakimzushia ni pamoja na kudai kuwa anajihusisha na ufugaji wa nguruwe na pia wanamtuhumu kuwa amebadilisha jina kinyemela na kujiunga na Ukristo.

Alisema kabla ya kutokea kwa vurugu hizo, baadhi ya waumini hao ambao walidhamiria kufanya uasi msikitini walikuwa wakikaa vikao vya kumshutumu mambo kadhaa kwa lengo la kumtaka aondoke na kuacha kusalisha katika msikiti huo, jambo ambalo alilikataa kwa sababu mambo yote yaliyokuwa yanaelezwa juu yake ni uzushi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bakwata wilaya ya Kyela, Daud Mwenda, alisema chanzo cha vurugu hizo ni baadhi ya vijana waliofukuzwa kutoka misikiti kadhaa nje ya mkoa wa Mbeya ambao wanataka kupindua uongozi uliopo.

source: nipashe
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan Tanzania Mpya untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Hisia za Mwananchi

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2013. Tanzania Mpya - All Rights Reserved
Template Modify by Hisia za Mwananchi
Proudly powered by Hisia