Mkazi wa kijiji cha Nyengedi mkoani Lindi, Khadija Hokororo (25), amejifungua mtoto wa kike huku midomo yake ikiwa imeungana.
Hali hiyo inamfanya mtoto huyo anyonye kwa shida maziwa na mama yake.
Habari zilizopatikana kijijini hapo zilieleza kuwa mtoto huyo alizaliwa katikazahanati ya kijiji hicho, Agosti 2, mwaka huu majira ya usiku.
NIPASHE lilifika kijijini hapo na kumshuhudia mtoto huyo midomo yake ikiwa imeungana na pua pamoja na matundu mawili sehemu ya mdomo wake.
Wakizungumza na NIPASHE kwa nyakati tofauti, baadhi ya wananchi pamoja na Afisa Mtendaji wa kata hiyo, Thomas Ngomo, walisema mtoto huyo alizaliwa katika zahanati ya Nyengedi, iliyopo katika kata hiyo kwa msaada wa muuguzi Elizabeth Raisi.
Aidha, walisema hilo ni tukio la kwanza kutokea kwa mtoto mwenye tatizo kama hilo kuzaliwa kijijini hapo.
Mama wa mtoto huyo, Hadija Rashid, alisema ni kama mkosi kwake ikizingatiwa ni kijana wake wa kwanza mwenye ulemavu kati ya watoto wake wawili.
“Huyu ni mtoto wangu wa pili, lakini huyu wa kwanza siyo kwa mume niliyenaye sasa...Mwenyezi Mungu ameamua kunijalia hivyo siwezi kumfanyia ubaya wowote kama wafanyavyo baadhi ya wanawake wenzangu. Nitamlea kama kawaida kwani yote yametokana na mapenzi yake Mungu,” alisema Khadija.
Alisema kwa sasa anatumia njia nyingine kumnywesha maziwa mtoto wake huyo ikiwamo kuyakamua na kuyaweka katika chombo kisha kummiminia kupitia kwenye matundu mawili yaliyopo eneo ambalo mdomo umeungana.
Mume wa mwanamke huyo, Salum Mnong’one, alisema baada ya kuzaliwa kwa mtoto huyo, walimpeleka katika hospitali ya Nyangao kwa msaada zaidi.
Hata hivyo, alisema wataalam wamemshauri ampeleke jijini Dar es Salaam katika Hospitali ya Kairuki kwa uchunguzi zaidi.
“Hivi sasa nipo katika kujitafutia nauli nimpeleke akapate tiba itakayomuwezesha mwanangu aweze kunyonya," alisema.
Aidha, muuguzi aliyemsaidia mama wa mtoto huyo kujifungua, Elizabeth, alisema hiyo ni mara yake ya kwanza kuzalisha mtoto akiwa na matatizo ya aina hiyo.

Source: Nipashe
0 comments:
Post a Comment