Home » » Hatimaye waziri Mwakyembe azungumzia skendo ya kupitshwa kwa madawa ya kulevya Uwanja wa ndege wa JK NYERERE

Hatimaye waziri Mwakyembe azungumzia skendo ya kupitshwa kwa madawa ya kulevya Uwanja wa ndege wa JK NYERERE

Hatma ya maofisa wanaoruhusu kupitishwa dawa za kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), imewadia kufuatia Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kuwaweka kitimoto viongozi wa idara nne watoe taarifa haraka ni kwanini uwanja huo umekuwa uchochoro wa kupitisha dawa hizo.


Pia amewataka maofisa hao kutoka idara ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Jeshi la Polisi na Usalama wa Taifa kutaja majina ya watumishi wanaohusika kula njama na wasafir
ishaji wa dawa za kulevya kupitia uwanja huo ili aweze kuwachukulia hatua haraka.



Dk. Mwakyembe ametoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya ofisi za wizara hiyo saa 11:30 jioni muda mfupi baada ya kumaliza kikao cha awali cha maofisa wa idara hizo.



“Bado naendelea na vikao, kifupi nimetaka maofisa wa TAA, Anga, polisi na Usalama wa Taifa wanipe taarifa haraka ni kwanini uwanja wa JNIA umekuwa uchochoro wa kupitishia dawa za kulevya,” alisema Dk. Mwakyembe.



Aliongeza: “nataka wataje wahusika wa biashara ya dawa za kulevya, nani aliacha mwanya hadi watu hao wakapita na dawa hizo, baada ya hapo nitachukua hatua.”



Kabla ya kuwaweka kitimoto maofisa wa idara hizo, Dk. Mwakyembe alifika katika uwanja wa JNIA kuzindua Kamati mpya ya Taifa ya Usalama wa Anga.



Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Fadhili Manongi alimweleza Dk. Mwakyembe kuwa changamoto ya ugaidi wa kimataifa imekuwa tishio kuu la usalama katika usafiri wa anga.



Julai 5, mwaka huu wasichana wawili wa Kitanzania walikamatwa nchini Afrika Kusini wakiwa na dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine kilo 150 zenye thamani ya Sh. bilioni 6.8,  zilizokuwa zikisafirishwa kutoka Tanzania.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan Tanzania Mpya untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Hisia za Mwananchi

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2013. Tanzania Mpya - All Rights Reserved
Template Modify by Hisia za Mwananchi
Proudly powered by Hisia