Licha ya ahadi na majigambo ya aina yake yaliyotolewa na kocha mkuu wa Taifa starz KIM POUSEN na achezaji wa Starz, Taifa starz ilikubali kichapo cha bao 3-1, kama ilivyokuwa katika mchezo wa awali uliofanyika wiki mbili zilizopita katika uwanja wa Taifa jijin Dar es salaam, Tanzania ilionekana kuwa dhaifu katika mchezo huo wa marudiano uliofanyka nchini Uganda huku wenyeji wakionesha uhai mkubwa.
Mchezo huo uliohusisha wachezaji wanaocheza wa ligi za ndani ulionesha wazi tofauti iliyopo kati ya soka la Tanzania na Uganda na hivyo kuifanya Uganda kuendelea kuwa wababe kwa Tanzania; wadau mbalimbali wameonesha kukrwa na matokeo ya mchezo huo lakini ni matokeo yaliyotarajiwa kutokana na udhifu ambao Taifa stars iliuonesha katika mchezo wa awali.
Hata hivyo kocha mkuu Kim poulsen kama kawaida yake hajakosa la kujijtetea alipodai kuwa wachezaji wake wamefungwa kutokana na wachezaji wengine nyota kuwa majeruhi; tanzaniampya.blogspot.com inawapa pole mashabiki wote wa Stars waliofadhaishwa na matokeohaya, hata hivyo inawaomba wasikate tamaa na waendelee kuipa sapoti stars.
0 comments:
Post a Comment