Home » » MAAJABU:"Askari Polisi warejesha fedha walizopora kwa mwananchi"

MAAJABU:"Askari Polisi warejesha fedha walizopora kwa mwananchi"

BAADHI ya askari polisi wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro, wamekiri kumpora mfanyabiashara madini sh milioni nne na kisha kuzirejesha.
Mfanyabiashara huyo aliyejulikana kwa jina moja la Darajani, inadaiwa aliporwa fedha hizo usiku wa Juni 3 mwaka huu, saa 1:45 akiwa katika kijiji cha Chirombola wilayani humo.
Hatua ya kurejeshwa kwa fedha hizo, imekuja baada ya gazeti hili kufichua tukio hilo hivi karibuni.
Taarifa zilisema kuwa askari hao walirejesha fedha hizo baada ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, kuagiza watuhumiwa wakamatwe na kushtakiwa, agizo ambalo halijatekelezwa hadi leo.
Chanzo chetu ndani ya polisi kilidokeza kuwa askari waliohusika katika tukio hilo walikiri kosa katika kikao kilichohusisha viongozi wa juu wa jeshi hilo wilayani humo, mfanyabiashara wa madini aliyeporwa na mfanyabiashara mwingine wa madini Maspana na Nasibu Mpanda.
Katika kikao hicho, inadaiwa kuwa polisi walitaka kumbebesha mzigo Mpanda maarufu kama Bob Nassa kuwa ndiye aliyehusika.
“Polisi walitaka kumsukumia kesi Bob Nassa, lakini alicharuka na kuwabana wafungue kesi ili akaseme ukweli kwani aliona wanataka kumzamisha,” kilisema chanzo.
Habari zaidi zilidai kuwa askari walikubali kurejesha sh milioni mbili na Maspana milioni mbili na kumtaka Darajani kuifuta kesi hiyo, jambo ambalo tayari limeshafanyika.
Alipohojiwa na gazeti hili, Darajani alikiri kuifuta kesi baada ya polisi kukiri kosa na kurejesha fedha hizo.
“Mimi nilipoona wamekubali kunirudishia fedha basi nikafuta kesi maana niliona italeta usumbufu kwangu. Kweli nimerejeshewa fedha zote,” alisema.
Wakati Polisi Ulanga wakiizima kesi hiyo kiana, Kamanda Shinogille aliliambia gazeti hili kuwa lazima wahusika wa tukio hilo wakamatwe na kufikishwa mahakamani.
“Nimeagiza huyo mfanyabiashara Maspana, askari na wote waliohusika wakamatwe na kufikishwa mahakamani,” alisema.
Katika tukio hilo lililotikisa wilaya hiyo na kijiji cha Chirombola, polisi hao walishirikiana na Maspana kumvamia Darajani na kufyatua risasi hewani kisha wakapora fedha hizo.
Kabla ya tukio hilo, Juni 2 saa nane usi
ku mmoja wa watuhumiwa Nasibu Mpanda alifika nyumbani kwa mama mzazi wa Darajani akitaka kujua sehemu anayolala mwanaye.
Habari zaidi zilisema kuwa baada ya kufika kwa Darajani, aligonga mlango na alipoitikiwa, alisema ametumwa na Maspana waende kufanya naye biashara ya madini.
Hata hivyo, Darajani aligoma kutoka nje na kumtaka Mpanda waonane kesho kwa ajili hiyo.
Ilipofika asubuhi ya Juni tatu saa 12 jioni, Darajani aliuza madini yake kwa mtu mwingine na kupata milioni nne.
Baada ya kuuza madini hayo akiwa na kitita chake cha sh milioni nne, Darajani aliamua kurudi nyumbani, lakini kabla hajafika alikutana na gari la Maspana na polisi wakampora fedha hizo.

source: Tanzania daima

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan Tanzania Mpya untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Hisia za Mwananchi

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2013. Tanzania Mpya - All Rights Reserved
Template Modify by Hisia za Mwananchi
Proudly powered by Hisia