CHANZO: NIPASHE
Wanafunzi watatu katika shule ya msingi Majimatitu jijini Dar es Salaam, `wamefanyiwa unyama wa kutisha’ baada ya kulawitiwa na kulazimishwa kula mbegu za kiume.
Watoto hao wenye umri wa miaka kati ya 9 na 10 (majina na madarasa yao yamehifadhiwa), walifanyiwa vitendo hivyo kwa mwaka mmoja, mhusika akidaiwa kuwa mkazi mmoja anayeishi jirani na shule hiyo.
Utafiti wa gazeti hili ulibaini kuwa mtuhumiwa wa uovu huo aliyejulikana kwa jina moja la Salum, alikuwa akifanya kitendo hicho ndani ya nyumba moja ya vyumba viwili, jirani na shule hiyo.
Mtuhumiwa huyo, anadaiwa kuwalipa watoto hao Shilingi 1,000 baada ya kuwalawiti na kuwaamuru wamsafishe sehemu zake za siri kwa kumnyonya.
WATOTO WASIMULIA
Watoto hao wameliambia NIPASHE Jumapili kuwa mtu huyo, alikuwa akiwafuata shuleni na kuwachukua hadi katika nyumba hiyo na kuwaingilia.
Walidai kuwa, walifanyiwa kitendo hicho mara mbili, asubuhi wakati wakienda shule na mchana wakati wa mapumziko.
Kutokana na muda mwingi wanakuwa na mtu huyo, walishindwa kuhudhuria masomo darasani kama wanavyofanya watoto wenzao.
"Huwa anakuja maeneo ya shule na kusimama nyuma ya mlingoti wa goli kwenye kiwanja cha mpira wa miguu, kisha anatuita kwa ishara ili tumfuate," alidai mtoto mmoja.
Alieleza kuwa baada ya kufika kwenye nyumba hiyo, watoto hao wanasimamishwa kwenye varanda kabla ya kuitwa mmoja mmoja kuingia chumbani.
"Anapotuita chumbani anatuambia tulale chini, anatulalia juu na kutulawiti, tukisikia uchungu anatuziba mdomo tusilie halafu anatutishia kutuua endapo tutamuambia mtu," alidai.
“anapomuingia mtoto mmoja na kumaliza, anamlazimisha kumlamba na kula mbegu zake za kiume kama njia ya kumsafisha ili aweze kumuita mtoto mwingine,” ilielezwa.
Pia, mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwa, akimaliza kuwalawiti, aliwapa chupa ya maji safi waende kujisafisha kabla ya kuwaruhusu kuondoka.
ILIVYOGUNDULIKA
Siri hiyo iligundulika baada ya mtoto mmoja kukutwa na wenzake akiwa na Shilingi 1,000, alipotaka kumpatia mwenzake Shilingi 200 za kununua mihogo.
Mariam Kimata, ni mzazi wa mmoja wa watoto hao, alisema alibaini tukio hilo kufuatia mwanafunzi mwenzake kwenda kumuuliza kama alimpa mtoto wake fedha za matumizi shuleni.
"Yule mtoto alikuja kwangu kuhoji kwa nini rafiki yake anakuwa na fedha nyingi wakati huu wa Ramadhan, nilishtuka sana nilidhani mtoto wangu ameanza tabia ya kuniibia," alisema.
Alisema, "kwa kawaida katika kipindi hiki baba yake hampatii fedha na kwa sababu amekuwa akitueleza amefunga."
Kimata, alisema mtoto wake aliporudi kutoka shuleni alimuhoji jambo hilo, mwanzo alikuwa akikataa na baadaye alikubali, lakini alisema aliokota njiani.
Hata hivyo, suala hilo lilifikishwa kwa baba wa mtoto huyo, ndipo alipoamua kusema ukweli kwa kuhofia kuchapwa voboko.
"Nilishtuka sana kiasi ambacho mapigo ya moyo yalishuka na kukimbizwa hospitali baada ya kusikia jambo hili baya," alisema.
HOSPITALI WATHIBITISHA
Kimata, alisema mumewe alimchukua mtoto huyo hadi kituo cha Polisi cha Charambe Majimatitu, kisha walipatiwa fomu ya PF3 kwa ajili ya kwenda hospitali ya wilaya ya Temeke.
Alidai kuwa daktari aliyemchunguza mtoto huyo alithibitisha kuingiliwa kinyume na maumbile na kupelekea njia ya haja kubwa kuharibika.
USTAWI WA JAMII YAZUNGUMZA
Afisa wa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Temeke, Sharifa Ally, alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo dhidi ya watoto hao wawili.
Hata hivyo, watoto hao waliruhisiwa baada ya kufanyiwa vipimo pamoja na kupatiwa matibabu.
"Tumelipokea tukio hilo, lakini wenzetu Polisi wanaendelea kulichunguza ili mtuhumiwa aweze kukamatwa," alisema.
SHULE YAKIRI KUZIDIWA
Uongozi wa Shule hiyo umejikuta katika hali tete baada ya kuzidiwa na vitendo vya wanafunzi wake kulawitiwa na watu wazima au wanafunzi wenyewe kwa wenyewe.
Mwalimu Mkuu msaidizi, Abel Masawe, alisema kitendo walichofanyiwa wanafunzi wake ni cha kinyama na kuiomba polisi kumkamata muhusika haraka.
Kwa mujibu wa Mwalimu Masawe, matukio ya aina hiyo yameongezeka kwa kasi shuleni hapo, kiasi ambacho inafikia watoto wenyewe wanafanyiana vitendo hivyo wakiwa nje ya eneo la shule.
Naye Afisa Elimu wa Manispaa ya Temeke, Honorina Mumba, aliahidi kulishughulikia suala hilo haraka iwezekanavyo.
Alisema kimsingi, mtuhumiwa lazima akamatwe kwa sababu amefanya kitendo cha kinyama kwa watoto hao.
MTUHUMIWA ASAKWA
Ingawa polisi katika mkoa wa kipolisi wa Temeke haujatoa tamko kuhusu tukio hilo, taarifa za uhakika zimeeleza kuwa jeshi hilo linaendelea kumsakata mtuhumiwa wa uovu huo.
0 comments:
Post a Comment