Home » » CCM sasa yaituhumu TUME YA KATIBA Kuwa haiwetendei haki

CCM sasa yaituhumu TUME YA KATIBA Kuwa haiwetendei haki

SOurce: gazeti la mwananchi
Dar es Salaam. 
                                                                                                                                                     
Katibu wa Itikadi na Uenezi (Nec-CCM), Nape Nnauye, ametuhumu Tume ya Mabadiliko ya Katiba k
uwa haitendi haki kwa kuwazuia wajumbe wa Baraza la Katiba kusoma waraka wa chama hicho unaopinga baadhi ya mambo yaliyopo kwenye rasimu.
Nape alitoa shutuma hizo jana alipozungumza kwa njia ya simu, alibainisha kuwa viongozi wa Jukwaa la Katiba akiwamo Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba, wanataka mapendekezo yaliyopo kwenye rasimu yapite yalivyo.
“Kwani kufanya hivyo wanazuia maoni ya wananchi, ingawa hatujawatuma kuusoma kwenye mapendekezo, lakini wana haki ya kuutumia wanavyojisikia,” alisema Nape.
Alisema wanajua wapo watu wachache wanaoupinga waraka huo wa CCM, lakini hawaelewi kwa sababu unahusu wanachama wao.
“Tume itende haki isikilize mawazo ya kila mtu, inachofanya sasa ni ubaguzi, wao wanatakiwa kusikiliza maoni siyo kutetea rasimu,” alisema.
Hivi karibuni vyombo vya habari viliripoti jinsi Jaji Warioba alivyokosoa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba wanaokwenda na matamko au nyaraka za vyama, badala ya maoni ya wananchi waliowachagua.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan Tanzania Mpya untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Hisia za Mwananchi

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2013. Tanzania Mpya - All Rights Reserved
Template Modify by Hisia za Mwananchi
Proudly powered by Hisia