Home » » WANANDOA WATIWA MBARONI KUMWUA MTOTO WAO, KISA UGOMVI WA MAPENZI

WANANDOA WATIWA MBARONI KUMWUA MTOTO WAO, KISA UGOMVI WA MAPENZI

Sumbawanga. 
Jeshi la Polisi katika Mkoa wa Rukwa linawashikilia wanandoa Livinus Choma (31) pamoja na mkewe Grace Choma (28) ambao ni wakazi wa Malangali kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mtoto wao ,Esther Choma (2) wakati wakipigana kutokana na wivu wa kimapenzi.
Kamanda wa Polisi Mkoa Rukwa, Jacob Mwarwanda alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Julai 22, saa 5:30 usiku baada ya rejea nyumbani, ulizuka ugomvi baina yao ambapo mwanamke alimtuhumu mume wake kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na wanawake wengine hali iliyozua ugomvi. baina yao
Alisema wakiwa wanapigana ghafla mume alimsukuma mke wake, ambaye aliteleza na kumuangukia mtoto huyo, ambapo baadaye alipoteza fahamu. Baada ya jitihada za kumpeleka hospitali kufanikiwa, mtoto huyo alifariki siku mbili baadaye kutokana na maumivu aliyoyapata
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan Tanzania Mpya untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Hisia za Mwananchi

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2013. Tanzania Mpya - All Rights Reserved
Template Modify by Hisia za Mwananchi
Proudly powered by Hisia