Baada ya malumbano ya mda mrefu kutokea kati ya wananchi wakishirikiana na makundi mbambali ya kijamii dhidi ya serikaali kuhusu kuanzishwa kwa kodi ya SIMKADI, Hatimaye serikali imesalimu amri na kukubali kurudisha mjadala huo bungeni ujadiliwe upya.
Awali mawaziri mbalimbali akiwemo waziri na naibu waziri wa mawasiliano na waziri wa fedha walitangaza na kutetea kwa msisitizo kuwa kodi hyo ni halali na ilipitishwa na wabunge ikiwa na lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kusambaza umeme vijijini hali iliyoleta jazba kwa wananchi na wanaharakati mbambali ikiwemo Wanasiasa kupitia vyama mbalimbali pamoja na CHADEMA, CCM, na vyama vingine ambavyo vilipinga waziwazi tozo hyo kwa madai kuwa inamwongezea mzigo mwananchi wa kawaida na kuwa haikufanyiwa utafiti na ushirikishwaji kwa walio wengi.
Hii inaweza kuwa habari njema kwa wananchi ambao kwa kiasi kikubwa walishitushwa na kauli za viongozi walioonekana kutetea kodi hyo iliyolalamikiwa na wengi.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
0 comments:
Post a Comment