Home » » POLISI: Hatukuwa na lengo la kumpiga BOMU Mnyika.

POLISI: Hatukuwa na lengo la kumpiga BOMU Mnyika.



Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limekanusha habari zinazosema kuwa wao walitaka kumpiga bomu mbunge wa ubungo John Mnyika lakini likamkosa.

Akizungumza kwa niaba ya Kamanda Kova, DCP Ali Mnenge amesema, Jeshi hilo lilikuwa katika doria za kawaida na hawakuwa na mpango wa kuzuia mkutano huo ila walitaka kujua kwanini wamekusanyika bila kibali.

DCP Mnenge amefafanua kuwa wakati wakiwa katika maongezi na mbunge huyo ili awatawanyishe wananchi hao, Askari aliyekuwa amebaki garini alikuwa akipanga vitu vizuri na ndipo bomu hilo la machozi lilipuka na mlio mkubwa kusikika.

Amesema hali hiyo ya mlipuko ilisababisha waliokusanyika katika mkutano huo kuhisi wana lengo la kumlipua na bomu kiongozi huyo wakati si kweli, pia ameongeza hakuna hata mtu mmoja aliyejeruhiwa.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan Tanzania Mpya untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Hisia za Mwananchi

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2013. Tanzania Mpya - All Rights Reserved
Template Modify by Hisia za Mwananchi
Proudly powered by Hisia